Mgomo wa wafanyabiashara Kariakoo walegea leo

 

Baadhi ya wafanyabiashara wa eneo la Kariakoo Jijini Dar es Salaam wamefungua maduka yao huku baadhi yao wakiendelea kufunga, kushinikiza kutatuliwa kero zao zilizopelekea kuitishwa kwa mgomo.

Hali hiyo imechangiwa na kauli ya Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Kariakoo, Martin Mbwana ya kuwaachia uamuzi wa kufunga au kufungua maduka katika eneo hilo mikononi mwa wafanyabiashara hao.

Wakati huo huo gari la matangazo limekuwa likipita leo mitaa tofauti ya Kariakoo kuhamasisha wafanyabiashara kufungua maduka yao, huku wakisisitiza kuwa kero mbalimbali zao zinaendelea kufanyiwa kazi.

Chapisha Maoni

0 Maoni