Serikali imependekeza kufanya marekebisho makubwa kwenye
Kanuni ya Ada na Tozo za Utalii ya mwaka 2015 ili kuleta mapinduzi makubwa
kwenye sekta ya utalii.
Akisoma hotuba yake
wakati akiwasilisha bungeni mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya mapato
na matumizi kwa mwaka 2024/2025 , Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt, Mwigulu Nchemba ameyataja
marekebisho kuwa ni pamoja na; kutoza ada ya Leseni za Biashara
za utalii kwa shilingi za Tanzania badala ya dola za Marekani.
Amesema mapendekezo haya
yanakwenda sambamba na kuweka
takwa la ada hizo kulipwa katika kipindi
cha miezi 12 kuanzia siku ya malipo ya mwisho ya leseni ya biashara
yalipofanyika.
Pia kupunguza ada ya leseni
ya biashara ya utalii inayolipwa na Wakala wa wapandisha watalii
mlimani kutoka dola za Marekani 2000 kwa mwaka hadi shilingi milioni 3
za Tanzania kwa mwaka.
Amefafanua kuwa lengo la hatua hizo ni kurahisisha mfumo wa ulipaji wa ada za utalii, kupunguza gharama za uendeshaji, kuvutia uwekezaji katika tasnia ya utalii na kuendana na matakwa ya kifungu cha 26 Cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania kinachoelekeza malipo yanayofanywa nchini kutumia shilingi ya Tanzania.
Na John Mapepele
0 Maoni