Prof. Muhongo aomba ujenzi wa viwanda 10 mkoa wa Mara

 

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, amesema katika miaka 60 hadi ya 90 mkoa wa Mara ulikuwa na viwanda, lakini kwa sasa hakuna kiwanda hata kimoja, na kuiomba Serikali  kiwanda kipya cha nguo, viwanda vitatu vya samaki, viwanda vya maziwa na viwanda vya kahawa.

Akichangia hoja bungeni leo Jijini Dodoma, Prof. Muhongo ameongelea bidhaa zinazozalishwa Mkoani Mara, na umuhimu wa ujenzi wa viwanda zaidi ya kumi (10) Mkoani humo, ambapo amesema katika kufanikisha mapinduzi ya viwanda mahala pa kuweka viwanda ni mkoa wa Mara.

"Sisi ni wakulima bingwa wa pamba tunaomba jineri zetu tatu zifanyekazi, tunaomba kiwanda kipya cha nguo, sisi ni wavuvi mashuhuri sasa hivi hatuna hata kiwanda kimoja cha samaki kilichopo kinafanya chini ya asilimia 15, ni wafugaji bingwa tunaomba viwanda vipya ya maziwa, Tarime tunalima kahawa tunaomba vile viwanda vipanuke zaidi," alisema Prof. Muhongo.

Vilevile, Mbunge huyo ametoa historia ya Mradi wa Liganga (chuma) na Mchuchuma (makaa ya mawe), na kuishauri Serikali iongeze kasi ya utekelezaji wa mradi huo muhimu kwa uchumi wa nchi.

Chapisha Maoni

0 Maoni