EU yaipatia tena fedha Tanzania kusaidia waathirika wa mafuriko

 


Umoja wa Ulaya (EU) umetoa msaada wa dharura wa kibinadamu wa shilingi 276,974,500 kuisaidia Tanzania kukabiliana na athari za mvua kubwa zilizoambatana na za El Nino zilizosababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi.

Msaada huyo wa fedha za mfuko wa dharura wa misaada ya kibinadamu, unalenga kuzisaidia familia zilizoathirika na mafuriko na maporomoko ya ardhi, ambayo yamesababisha vifo watu na kuharibu maelfu ya makazi.

Fedha hizo ni nyongeza ya fedha shilingi 276,974,500 zilizotolewa awali kwa Shirika la Msalaba Mwekundu Tanzania (TRCS) mwezi Desemba 2023, ambazo zilitolewa na EU kusaidia kukabiliana na mafuriko na kufanya jumla ya msaada sasa kuwa shilingi 553,949,000.

Taarifa iliyotolewa leo imesema EU itaendelea kuiunga mkono TCRS katika kutoa msaada unaohitaji kwa haraka, kuimarisha uokoaji wa maisha ya watu na misaada ya dharura kwa walioathirika mno, hususana watu ambao nyumba zao zimeharibika na wale waliolazimika kukimbia makazi yao.

Msaada huo wa fedha wa ziada utatoa fursa kwa Shirika la Msalaba Mwekundu Tanzania, kuimarisha utoaji misaada kwa watu 85,000 katika sehemu mbalimbali za Tanzania ikiwamo Morogoro, Mbeya, Kilimanjaro, Unguja, Geita, Dar es Salaam, Manyara na Pwani.

Chapisha Maoni

0 Maoni