KLABU ya mazoezi ya Bondwa Hiking ya Mkoani Morogoro kwa
kushirikiana na jeshi la polisi Mkoani humo limefanya matembezi ya Kms 15 na
mbio za Hisani Kms 30 lengo likiwa ni kuunga mkono wito wa waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa la kuwata wananchi
kushiriki mazoezi ya ili kuweza kupambana na magonjwa mbalimbali yasio
ambukiza.
Mbio hizo ziliongozwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda
Ya Morogoro Mhe. Latifa Mansoor kwa kushirikiana na maafisa askari wa jeshi la
Polisi, watumishi wa Mahakama pamoja na baadhi ya joking club zilizopo mkoani humo.
Aidha, katika mbio hizo kuligawanyika kundi jingine ambalo
lilotembea umbali wa Km 15 kuzunguka maeneo tofauti ya Ndani ya Manispaa ya
Morogoro.
Akizungumza wakati wa kuhitimisha mbio na matembezi hayo
Jaji wa Mahakama Kuu kanda ya Morogoro Latifa Mansoor aliipongeza Club ya
Bondwa Hiking Club pamoja na jeshi la polisi kwa kuweza kushirikiana katika
kuandaa tukio hilo hali ambayo limesaidia kuimarisha afya ya mwili pamoja na
akili.
Hata hivyo Mhe Latifa
Mansoor amesema kuwa Klabu hiyo imewapa hamasa na wao kama Mahakama sasa
watakuwa wakishirikiana na Jeshi la polisi Kila Jumamosi ya Mwisho wa mwezi
katika kufanya mazoezi ya pamoja.
Akimuwakilisha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Afisa
mnadhimu wa jeshi la polisi Mkoani humo ACP Yohana Mjengi amesema kuwa jeshi
hilo litaendelea kufanya maoezi ya pamoja kila mwisho wa mwezi ili kuimarisha
afya zao.
Aidha amepongeza ushirikiano ulionyeshwa na Klabu ya Bondwa
katika maandalizi hadi kufanyika kwa mbio pamoja na matembezi hayo ambayo
yalikuwa na lengo kuunga kwa vitendo kauli mbiu ya waziri Mkuu Kassim Majaliwa
ambayo ailiitoa mapema mwezi huu.
Kwa upande wake Wakili Mwansoho ambae ni mwenyekiti wa Club
ya Bondwa hiking amesema kuwa licha ya wao kujiunga kwa pamoja katika kufanya
mazoezi ili kupambana magonjwa yasiyo ambukizwa pia wamekuwa wakihamasisha
utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji.
Sanjari na hilo ameeleza kuwa klabu hiyo imekuwa akitoa misaada mbalimbali kwa watu wasiojiweza na wenye mahitaji maalumu.
Nae Mratibu wa Club hiyo George Matiku amesema kuwa
takribani askari zaidi ya 90 wa Kikosi cha Kutuliza Ghasi waliweza kushiriki mbio
za km 30 huku Zaidi ya Askari 120 wakishiriki katika matembezi ya KMs15 huku
Makamu Mwenyekiti Juma Mbonde akieleza kuwa tangu kuanza hadi kumalizika kwa
matembezi na mbio hizo hakuna aliyepa majeraha yeyote hivyo wote waliweza
kumaliza salama.
Katika zoezi hilo kijana mwenye Umri wa miaka 12 wa Darasa la Sita Ally Silim Seif aliweza kumaliza mbio za Kms 30 ambapo amewataka watoto wenzie kujikita katika kufanya mazoezi kwani pia inasaidia kuimarisha uwezo wa kufikiri hasa katika masomo yao.
0 Maoni