Dk. Biteko kufungua Mkutano wa 13 wa Mwaka wa Kitaaluma wa TEF kesho

 

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) litafanya Mkutano wa 13 wa Mwaka wa Kitaaluma kwa siku mbili kuanzia kesho tarehe 29/04/2024 Jijini Dodoma.

Akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma Mjumbe wa Kamati ya Utendaji TEF, Neville Meena amesema mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko.

Kauli mbiu ya Mkutano wa 13 wa Mwaka wa Kitaalum wa TEF ni “Uandishi wa habari kuhamasisha matumizi ya gesi kulinda misitu”.

Chapisha Maoni

0 Maoni