Watumishi wanawake wa Wakala ya Barabara za Vijijini na
Mijini (TARURA) wamepongezwa kwa kuwawezesha wanawake wenzao waliopo kwenye
gereza la wanawake la Isanga jijini Dodoma.
Wanawake wa TARURA wametembelea gereza la wanawake Isanga leo
ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanayofanyika Machi
8, kila mwaka
Kamishna Msaidizi wa Magereza na Mkuu wa Gereza Kuu-lsanga,
Dodoma ACP. Zephania Neligwa amewapongeza wakati alipokea mahitaji mbalimbali
kutoka kwa watumishi wanawake wa TARURA Jijini Dodoma.
ACP. Neligwa amesema mahitaji hayo yataenda kuwasaidia
wanafunzi wao ambao ni wafungwa na mahabusi waliopo mafunzoni katika gereza la
wanawake na kuongeza kwamba mahitaji hayo yatatumika ipasavyo.
“Mnapokuwa mnaadhimisha siku ya wanawake duniani sisi
magereza tunaendeleza programu za
urekebu kwa kuwajengea uwezo na ujuzi mbalimbali wanawake hawa ili hata
watakaporudi uraiani waendelee kuzalisha na kuwa wajasiliamali”.
Naye, Afisa Utumishi wa TARURA Bi. Ntuli Mwasalyanda amesema
wao kama watumishi wanawake wanapoelekea kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani
wameona ni vyema kuwagusa/kuwafikia wanawake wenzao waliopo gereza la wanawake
–Isanga.
“Tumeona ni jambo jema kuadhimisha siku ya wanawake duniani na wanawake hawa ili wajione kwamba
nao ni sehemu ya wanawake waliopo uraiani, watambue kuwa jamii haijawatenga na
ipo nao, tumefurahi kwa kuona wanajishughulisha na shughuli mbalimbali”.
Bi. Ntuli ameongeza "Tumefurahi namna wanawake hawa
walivyowezeshwa kwa kufanya stadi mbalimbali za mikono ambazo zinawaletea
maendeleo ikiwemo ujuzi baada ya kutoka magereza.
Kwa upande wake, Mratibu wa Magereza na Mkuu wa sehemu ya
wanawake SO. Sifa Anyimike amewashukuru watumishi hao wanawake wa TARURA.
"Kwa kuwatembelea wanafunzi waliokinzana na Sheria
katika gereza hili," amesema.
Amebainisha lengo la mafunzo wanayoyapata wanawake hao ni
kuwasaidia watakaporudi uraiani kwa
kuwawezesha kujiunga na vikundi vingine vya wanawake wajasiliamali.
0 Maoni