Kamanda Mkuu wa Idara Maalum za Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali
Mwinyi amewahimiza Maafisa, Askari na Wapiganaji wa Vikosi vya Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar kuendelea kudumisha nidhamu, uzalendo, uwajibikaji na
uadilifu.
Rais Dk. Mwinyi amesema hayo akizungumza na Maafisa , Askari
na Wapiganaji alipotembelea Kikosi cha Kuzuia Magendo Zanzibar (KMKM) Kibweni
na Kikosi cha KVZ Mtoni Mkoa wa Mjini
Magharibi ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea Vikosi vya SMZ na kuhitimisha leo tarehe: 10 Machi 2024.
Aidha, Rais Dk. Mwinyi amewapongeza Kikosi cha Kuzuia Magendo
(KMKM) na Kikosi cha KVZ kwa utekelezaji wa kazi nzuri za ujenzi wa miradi
mbalimbali ya maendeleo inayofanywa na Serikali.
Kwa upande mwingine, Rais Dk. Mwinyi amesema Serikali
itaendelea kuboresha miundombinu mbalimbali ya vikosi hivyo.
0 Maoni