Habari zilizotufikia zinaeleza kuwa boti ndogo inayofanya
utalii wa majini na kuvua samaki imezama baharini katika eneo la Coco Beach Jijini
Dar es Salaam.
Taarifa za awali zinaonesha kwamba boti hiyo ilikuwa na watu
tisa na wote wameokolewa.
Jeshi la zimamoto na uokoaji kwa kushirikiana na polisi
wanamaji wanaendelea na zoezi la kuivuta boti hiyo.
0 Maoni