Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
Freeman Mbowe, amekanusha madai ya kuahidiwa nafasi ya uwaziri mkuu na kusema kuwa
nafasi hiyo haitolewi kama keki wala mkate, huku akisisitiza kuwa bado ana
nguvu na hajachoka.
Mbowe amezungumza hayo leo Jumamosi Desemba 21, 2024
nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam, alipokutana na wahariri na
waandishi wa habari, kama alivyotoa ahadi yake na kujipa muda wa saa 48.
“Uwaziri mkuu hautolewi kama keki, au mkate, uwaziri mkuu
ni suala la kikatiba kwa hiyo viongozi wenzangu nategemea mkizungumza mzungumze
mambo ambayo yatatuonyesha kama taasisi makini,” alisema Mbowe.
Hili jambo siyo kweli sijawahi kulizungumza mahali
popote, sijawahi kujadiliana na yeyote wala sijawahi kupewa zawadi ya cheo,
napataje cheo cha bure, alisema Mbowe.
Sijui wanatumia kigezo gani kusema Mbowe amechoka, aisee
mimi sijachoka wewe. Naweza kufanya mikutano minane kwa siku bila kula.
Nionyeshe nani anaweza hivyo, alijigamba Mbowe.
0 Maoni