Wananchi waliokubali kuhama kwa hiari kutoka ndani ya
Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Kijiji cha Msomera Handeni Tanga
wameendelea kunufaika na upatikanaji wa mahindi yanayotolewa na Serikali
kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Lengo la ugawaji wa mahindi hayo ni kuwasaidia wananchi
waliohamia kijijini hapo hivi karibuni kupata chakula kwa miezi 18 ijayo wakati
wakiendelea kuandaa mashamba kwa ajili ya kilimo.
Kaya 125 zimegawiwa mahindi gunia mbili kwa kila kaya
ambapo Kaya hizo zinajumuisha kaya 23 zilihamia Msomera tarehe 19 Desemba,
2024.
0 Maoni