Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi
Chana (Mb) amewaasa watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi zake
kutekeleza majukumu yao kwa ubunifu katika kuendeleza Sekta ya Maliasili na
Utalii.
Ameyasema hayo leo Desemba 21, 2024 katika Mkutano wa 32
wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika ukumbi wa Mikutano wa Kituo cha Utalii
Ngorongoro jijini Arusha.
"Lazima tufanye kazi za Watanzania ambao wametupa
dhamana kwa ari na ubunifu wa hali ya juu," Mhe. Chana amesisitiza.
Aidha, ameitaka menejimenti ya Wizara ya Maliasili na
Utalii kuhakikisha inaendelea kusikiliza madai na changamoto za Utumishi na
kuzitatua.
Amewataka kutumia fursa ya baraza hilo kujadili hoja za
kiutumishi, mustakabali ya hali za Utumishi na utekelezaji wa malengo ya Sekta
ya Maliasili na Utalii.
Katika hatua nyingine Mhe. Chana ameielekeza menejimenti
na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuweka mazingira
wezeshi kuvutia wawekezaji,Kusimamia na kulinda malikale kwa manufaa ya Taifa
na kuimarisha usimamizi na ulinzi wa rasilimali kwa faida ya kizazi cha sasa na
baadaye.
Naye, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Dkt.
Hassan Abbasi amesema Wizara imeendelea kuweka kipaumbele changamoto na maslahi
ya watumishi sambamba na kuweka mazingira wezeshi ya utendaji kazi.
"Tunahakikisha kila panapowezekana tunakwenda
vizuri, Serikali yetu inaendelea kutuwezesha kwa hiyo kazi inapaswa kuendelea,"
amesema Dkt. Abbasi.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Menejimenti ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Maliasili na Utalii, Viongozi wa wa TUGHE Taifa na Mkoa pamoja na watendaji kutoka Taasisi za Wizara ya Maliasili na Utalii.
Na. Happiness Shayo - Arusha
0 Maoni