Halmashauri 112 hazina maambukizi mapya ya mabusha na matende

 

Serikali kupitia Wizara ya Afya imesitisha kampeni ya umezeshaji wa kinga tiba za ugonjwa wa mabusha na matende katika Halmashauri ya Jijini la Da es Salaam, Manispaa ya Temeke na Kata 10 za Manispaa ya Kinondoni ambazo hazina maambukizi mapya ya ugonjwa huo.

Waziri wa Afya Mhe.  Ummy Mwalimu amesema hayo jana Machi 12, 2024, wakati akiongea na wandishi wa habari juu ya hatua zilizofikiwa za kutokomeza ugonjwa wa mabusha na matende nchini hususan katika Mkoa wa Dar es Salaam.

“Serikali kwa kushirikiana na wadau tumeweza kudhibiti ugonjwa huu katika Halmashauri 112 kati ya 119 na kubakiwa na Halmashauri 7 ambapo mafanikio hayo yamechangiwa na kampeni za utoaji elimu na umezaji kinga tibaza ugonjwa  huo zilizofanyika katika maeneo mbalimbali yanchi,” amesema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy amesema bado kuna baadhi ya Halmashauri ambazo bado zina maambukizi mapya ya ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na Pangani, Mafia, Kinondoni,  Kilwa, Lindi Manispaa, Mtamana Mtwara Mikindani ambapo kwa ujumla kata hizo zinawakazi 1,203,359.

"Natoa rai kwa wakazi wa maeneo hayoa mbayo bado kuna maambukizi ya ugonjwa huu kujitokeza kwa wingi ili kushiriki kwenye kampeni za kinga tiba ya ugonjwa wa matende na mabusha zitakazoendelea kufanyika katika maeneo yao ilikuweza kutokomeza maambukizi mapya ya ugojwa huu," amesema Waziri Ummy.

Amesema, Kigamboni na Ubungo hazina maambukizi mapya kwa kipindi cha miaka sita baada ya kusitisha umezaji wa kingatiba huzo hatua iliyowezesha watu milioni 3.7 kuokolewa katika hatari ya kupata maambukizi mapya jijini Dar es Salaam.

Waziri Ummy amemshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kujali afya zaWatanzania ambapo amewezesha upatikanaji wa fedha pamoja na vifaa katika kufikia mafanikio hayo.

Kwa upande wake, Mratibu Udhibitiwa Ugonjwa wa Matende na Mabusha Wizara ya Afya, Dkt. Faraja Lyamuya amesema sababu zinazochangia maambukizi mapya katika baadhi ya maeneo ni jamii kutokuwa na uelewa wakutosha pamoja nak uhamahama hali inayosababisha kutoshirikiki kamilifu katika umezaji wa kinga tiba.

Kuhusu maambukizi mapya kuwepo katika maeneo ya Pwani zaidi amesema ni kwa sababu ya hali ya hewa na mazingira ambayo huruhusu mazalia ya mbu na kwamba maeneo ya mazalia yenye mbu wengi ndiyo yalionekana kuwa na kiwango cha juu cha maambukizi.

Tathmini inaonyesha kambi ya mwisho ya upasuaji wa mabusha na matende ilifanyika mwaka 2023 na kuvu kalengo la kufanya upasuaji kwa zaidi yawatu 1,100.

Chapisha Maoni

0 Maoni