Wakulima wa Mpunga Kata ya Madibira wilaya ya Mbarali Mkoani
Mbeya wameishukuru Serikali ya Rais wa Awamu ya Sita chini ya Mhe. Dkt. Samia
Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji wa mifereji ya Umwagiliaji Mashamba ya Mpunga Madibira kupitia Mradi wa
Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii REGROW,
kwa kuwa mradi huo unawawezesha kulima mpunga kuwa na uhakika wa kupata mavuno
wanayotarajia.
Wakulima hao wametoa pongezi hizo kwa Mhe. Rais Samia akiwa
anatimiza miaka mitatu tangu aanze kuiongoza Serikali ya Awamu ya Sita ambapo
wameeleza kuwa mradi huo umeanza kuwaletea tija kwani kwa sasa kwani wakilima
Ekari mbili na nusu wanapata tani 12 hadi 15 ambapo zamani walikuwa wakipata
tani nne mpaka tani saba kutokana na changamoto ya ukosefu wa maji ya uhakika.
Aidha, wanufaika wa mradi wa umwagiliaji wa Skimu ya
Umwagiliaji ya Madibira inayotekelezwa kupitia REGROW chini ya Wizara ya
Maliasili ambapo wananchi wanaishukuru serikali kwa kutimiza ahadi ya
uendelezaji kilimo cha umwagiliaji chenye matumizi rafiki ya maji.
Kadhia ya ugomvi wa mara kwa mara huku wakiwa wamebeba silaha
aina ya panga kuyatafuta maji wameondokana nayo na na kukiri kuwa utekelezaji
wa mradi huu umesaidia upatikanaji maji ya uhakika na kuweza kuendesha kilimo
wakiyasubiria kwa shahuku kubwa mavuno yao huku amani ikitawala.
Mradi huo unatekelezwa na Wakandarasi Wazawa kutoka katika
Kampuni ya Skyline Properties Limited kwa kushirikiana na White City International
kuwa wataendelea kutekeleza miradi kwa kiwango kimachopaswa huku Mhandisi wa
Umwagiliaji skimu ya Madibira Njanji Mlwale amesema ufanisi katika kusafirisha
maji utakuwa bora kuliko kipindi cha nyuma.
0 Maoni