Katika kukabiliana na mlipuko wa kipindupindu nchini Tanzania,
Umoja wa Ulaya (EU) umetenga kiasi cha Euro 150,000 sawa na shilingi milioni
414 za Tanzania kwa ajili ya misaada ya kibinadamu.
Msaada huo wa Umoja wa Ulaya unalenga katika kuisaidia Tanzania
kuudhibiti mlipuko wa kipindupindu, ambao unahatariasha maisha ya watu milioni
4 katika mikoa iliyokumbwa na ugonjwa
huo.
Taarifa iliyotolewa leo Machi 4, 2024 na Umoja wa Ulaya
imesema mlipuko wa kipindupindu unazidi kushika kasi kwenye mikoa 13 ya
Tanzania, ambayo ilipatwa na ugonjwa huo tangu Januari 2024.
Takwimu zinaonyesha kuwa watu 1,500 wameugua ugonjwa huo wa
kipindupindu ambapo miongoni mwao 34 wamefariki dunia. Msaada huo wa EU utatumika
kwa miezi mitatu hadi mwishoni mwa Mei 2024.
0 Maoni