Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar mpya itakuwa na usafiri wa umma wa
mabasi ya umeme, treni pamoja na Taxi za baharini.
Amesema Serikali itatiliana saini mradi wa kituo cha usafiri
wa baharini eneo la Mpiga Duri tarehe 09 Januari 2024.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipoweka Jiwe la Msingi la
Ujenzi wa Soko kuu la Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi B , Mkoa wa Mjini
Magharibi tarehe: 06 Januari 2024 katika shamrashamra za Miaka 60 ya Mapinduzi
ya Zanzibar.
Aidha Rais Dkt.Mwinyi amesema ametimiza ahadi aliyoitoa kwa
wafanyabiashara wakati wa kipindi cha kampeni za uchaguzi Mwaka 2020 ikiwemo
kuwajengea mazingira bora ya kufanyia biashara, kuwawezesha kwa mitaji na vitendea
kazi.
Vilevile ameeleza
Serikali imetimiza ahadi yake kwa kutoa mikopo inayofikia bilioni 25
kuwawezesha wajasiriamali nchini na halikadhalika wavuvi, wakulima wa mwani
wamepatiwa boti bila kuwasahau waendesha bodaboda.
Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi ametoa kipaumbele kwa wafanyabiashara wa awali wa soko la Mwanakwerekwe baada ya kukamilika Mwezi Machi kati ya wafanyabiashara 5,000 watakaoingia kwenye soko hilo.
0 Maoni