Rais Dk. Mwinyi avitaka vyuo kuongeza programu za uchumi wa buluu

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema kazi inayofanywa na taasisi za elimu ya juu ni kielelezo cha  mchango wa sekta binafsi  kuchangia maendeleo ya Zanzibar kwa kuandaa wataalamu wa fani mbalimbali.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo katika Mahafali ya 23 ya Chuo Kikuu cha Abdulrahman Al -Sumait Chukwani, Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe: 27 Januari 2024.

Aidha Rais Dk.Mwinyi amepongeza juhudi zinazofanywa na Chuo hicho kinachomilikiwa na Shirika la Direct Aid ya Kuwait kwa mchango wake katika maendeleo ya sekta ya elimu Zanzibar tangu kuanzishwa kwake 1998.

 Rais Dk. Mwinyi amevihimiza vyuo kujikita katika utafiti utakaotoa ufumbuzi wa changamoto zinazoikabili jamii kwa kushirikiana na taasisi na idara mbalimbali za Serikali.

Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amevitaka vyuo kikuu kuongeza programu zinazoakisi mahitaji ya nchi ikiwemo zinazohusu uchumi wa buluu.

Mahafali hayo yamehudhuriwa na Mkuu wa Chuo cha Abdulrahman Al-Sait, Rais Mstaafu Mhe.Dkt Amani Abeid Karume, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Lela Mohamed Mussa , Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi  Mhe.Idrissa Kitwana Mustafa pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali, wa Dini na Vyombo vya ulinzi na usalama.


Chapisha Maoni

0 Maoni