Mama aliyejifungua mapacha walioungana ampongeza Rais Samia

 

Bi. Mariam Shabani, Mkazi wa Kigamboni, aliyejifungua watoto pacha walioungana na kisha kutenganishwa  hivi karibuni na Hospitali ya Taifa Muhimbili amempongeza na kumtakia heri  Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika siku yake ya kumbukizi ya kuzaliwa.

Aidha, amempongeza Mhe. Rais Dkt. Samia kwa uwekezaji katika Sekta ya Afya hususani Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Mohamed Janabi amewahakikishia Watanzania kuwa watanufaika (returns) na huduma bora kutokana na uwekezaji uliofanywa na Serikali Hospitalini hapo.

Kutokana na uwekezaji huo wa Serikali Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wamefanikisha upasuaji huo wa kibingwa na mama na watoto wake wanaendelea vizuri.



Chapisha Maoni

0 Maoni