Mafuriko yaua watu watatu wa familia moja Morogoro

 

Mvua zilizonyesha usiku wa kuamkia leo Januari 10, 2024 na kupelekea kufurika Mto Mgolole Manispaa ya Morogoro, zimesababisha vifo vya watu watatu wa familia moja akiwemo bibi, mama na mjukuu huku baba wa familia hiyo Sengo Hamis akijeruhiwa

Baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo wameelezea kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa nane usiku wa kuamkia leo, ambapo kufuatia mafuriko hayo nyumba ya familia hiyo ilizingirwa na maji na wakati wakijiokoa kuvuka mto maji yakawazidi nguvu na kusowasomba.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa Morogoro Mrakibu wa Zimamoto Shabani Marugujo, amesema hadi sasa wamefanikiwa kuopoa miili ya watu wawili ukiwemo wa mjukuu aliyefahamika kwa jina la  Asnath (6) na bibi aliyefahamika kama Thelesia Adroph anayekadiriwa kuwa na umri miaka 70 -76 huku jitihada za kuutafuta mwili wa Mwanahamis Issa zinaendelea.

Chapisha Maoni

0 Maoni