Timu ya taifa ya Cape Verde imeifunga Ghana magoli 2-1 katika tukio ambalo limeushangaza ulimwengu wa soka kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2023, inayoendelea nchini Ivory Coast.
Katika mchezo huo Cape Verde ilikuwa ya kwanza kutikisa nyavu za Ghana kupitia kwa Monteiro Alvarenga katika dakika ya 17 ya mchezo, ambapo Ghana walisawazishwa katika kipindi cha pili kupitia kwa Djiku mnamo dakika ya 56.
Wakati Ghana wakidhani kuwa mchezo huo unaishia kwa sare Cape Verde walipata goli la pili katika dakika za mwisho za mchezo kupitia kwa Mendes Rodrigues na kulizamisha jahaza la Ghana timu ambayo ilikuwa inapewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo.
Katika michezo mengine jana Nigeria nayo ilijikuta ikiwa katika wakati mgumu baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Equatorial Guinea, huku nao Mafarao wa Misri wakitolewa jasho na Msumbiji katika mchezo ulioishia kwa sare ya magoli 2-2.
0 Maoni