Dk. Nchimbi arithi mikoba ya Chongolo CCM

 

Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana leo mjini Unguja, Zanzibar, imemteua Dk. Emmanuel John Nchimbi kuwa Katibu Mkuu mpya wa CCM.

Uteuzi wa Dk. Nchimbi umefanyika leo Januari 15, 2024 katika Kikao cha Kamati Kuu ya CCM, na kisha kuthinbitishwa na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC).

Dk. Nchimbi anachukua mikoba ya Ndugu Daniel Godfrey Chongolo aliyejiuzulu wadhifa wa Katibu Mkuu wa CCM, Novemba mwaka jana kwa madai ya kuchafuliwa kwenye mitandao ya kijamii.

Chapisha Maoni

0 Maoni