OSHA yawa mfano wa kuigwa katika nchi za Afrika

 

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama Mahala Pa Kazi (OSHA) Khadija Mwenda akizungumza na Jukwaa la Wahariri (TEF) pamoja na Waandishi wa Habari kuhusu mafanikio ya OSHA kwa miaka mitatu ya awamu ya sita ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, mkutano huo umefanyika jana Jijini Dar es Salaam. Mwenda amesema baadhi ya mataifa ya Afrika yamekuwa yakija kujifunza utendaji OSHA.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji TEF Jane Mihanji akitoa mchango wake katika mkutano wa OSHA na Wahariri pamoja na Waandishi wa Habari, uliofanyika kuelezea mafanikio ya OSHA chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina.

Afisa Habari Mwandamizi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina Sabato Kosuri akizungumza kuhusiana na uratibu wa mikutano hiyo ya taasisi za umma zilizo chini ya Ofisi ya Msajili Hazina kueleza mafanikio na utendaji kazi zao kwa vyombo vya habari.

Baadhi ya washiriki wa Mkutano huo wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama Mahala Pa Kazi (OSHA) Khadija Mwenda, wakati akielezea mafanikio ya OSHA, kwenye mkutano uliofanyika Jijini Dar es Salaam.

Chapisha Maoni

0 Maoni