TTB wasisitizwa kuzingatia uadilifu na kuwajibika

 

Naibu Waziri Wizara ya Maliasili na Utalii, Mhe. Dunstan Kitandula (Mb) akiwasisitizia wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kuwa waadilifu na wawajibikaji katika kutekeleza majukumu yao. Mhe. Kitandula ameyasema wakati anafungua rasmi kikao cha tano cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika Mkoani Iringa.


Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la TTB wakisikiliza ujumbe unaotolewa na Naibu Waziri Wizara ya Maliasili na Utalii, Mhe. Dunstan Kitandula (Mb) wakati akifungua rasmi kikao cha tano (5) cha Baraza la Wafanyakazi la TTB.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTB, Mhe. Balozi Dkt. Ramadhani Dau akiahidi kuwa Bodi ya Wakurugenzi pamoja na Menejimeneti watahakikisha wanabuni mikakati ya vyanzo vya mapato ili Bodi iweze kuwa na vyanzo vingine vya mapato.

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi TUICO Tawi la TTB, Wiliam Halule akichangia hoja wakati wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika mkoani Iringa.

Chapisha Maoni

0 Maoni