Mloganzila yaunganisha mifupa ya taya na uso iliyovunjika

 

Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila imefanya upasuaji wa kuunganisha mifupa ya taya na uso iliyovunjika kwa mtu aliyepata  ajali.

Daktari Bingwa wa Kinywa na Meno Muhimbili Mloganzila Dkt. Dominicus Kabogo amesema kufanyika kwa upasuaji huo kutasaidia kuleta ufanisi wa kutafuna, kuongea na mgonjwa kurejesha muonekano mzuri wa uso.

Chapisha Maoni

0 Maoni