Mfumo wa NeST kuziba mianya ya rushwa- Mhe. Ridhiwani

 

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete  anesema eneo la ununuzi wa umma limekuwa likiripotiwa kugubikwa na vitendo vya rushwa na ubadhirifu ambapo  zaidi ya asilimia 72 ya bajeti ya Serikali imekuwa ikitumika kwenye manunuzi  hayo ya umma.

Amesema kutokana na  uzito huo  Serikali kupitia Mamlaka ya Serikali Mtandao imeamua kusanifu, kujenga na kusanikisha Mfumo wa Kitaifa wa Kielektroniki wa Ununuzi Tanzania {National e-Procurement System of Tanzania (NeST)} ili kuweza kukabiliana na changamoto hiyo.

Mhe. Kikwete ametoa kauli hiyo leo Jijini Arush wakati akifunga  kongamano  la 14 la mwaka la wataalam wa ununuzi na ugavi zaidi ya 900 lenye kauli mbiu "Mabadiliko ya kidijitali kwa ajili ya kuboresha usimamizi na ugavi kelekea maendeleo endelevu".

Amesema mfumo huo utasaidia  kuondoa mianya ya rushwa na upendeleo na hivyo thamani ya pesa za Serikali katika bidhaa na huduma italindwa kwani kutakuwa hakuna  ulazima wa  watu kukutana ana kwa ana.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Ridhiwani Kikwete akiwa kwenye picha  ya pamoja na baadhi ya viongozi na watendaji mara baada ya kuwasili kufunga  kongamano  la 14 la mwaka la wa ununuzi na ugavi uliofanyika Jijini Arusha


Chapisha Maoni

0 Maoni