Majaliwa amwakilisha Rais Dkt. Samia sherehe za kumwapisha Rais Rajoelina wa Madagascar

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi katika sherehe za kumwapisha Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina zilizofanyika kwenye uwanja wa michezo wa  Barea uliopo Mahamasina, Desemba 16, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi katika sherehe za kumwapisha Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina wa Madagascar   zilizofanyika kwenye uwanja wa michezo wa  Barea uliopo Mahamasina, Desemba 16, 2023. Kushoto ni mkewe Mama Mary Majaliwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Rais wa Comoro, Azali Assoumani akisalimiana na Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa katika sherehe za kumwapisha Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina zilizofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Barea uliopo Mahamasina, Desemba 16, 2023. Kulia ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina akiwapungia wananchi alipowasili kwenye uwanja wa michezo wa Barea uliopo Mahamasina kuapishwa kuwa Rais wa nchi hiyo kwa kipindi cha tatu, Desemba 16, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina akihutubia Taifa baada ya kuapishwa kuwa Rais wa nchi hiyo kwa kipindi cha tatu katika sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Barea uliopo Mahamasina, Desemba 16, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina akiwa na mkewe, Mialy Rajoelina, na watoto wao Arena Rajoelina na Ilonstoa Rajoelina (kulia) baada ya kuapishwa kuwa Rais wa nchi hiyo kwa kipindi cha tatu katika sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Barea uliopo Mahamasina, Desemba 16, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Chapisha Maoni

0 Maoni