Umoja wa Mataifa wasema watoto 160 wanauawa kila siku Gaza

 

Msemaji wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, ameeleza kuwa kumekuwapo na matukio ya vifo kwa pande zote mbili za Gaza na Isarel, na kusema kwa wastani watoto 160 wanauawa kila siku Gaza.

Mapema Shirika la Afya Duniani (WHO) lilisema kiwango cha matukio ya vifo na mateso katika vita hiyo baina ya Israel na Hamas ni vigumu kuingia akilini.

Wakati huo huo Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant amesema vikosi vya nchi hiyo vipo katika maeneo ya kati ya Mji wa Gaza.

Gallant amesema vikosi vya Israel vimeingia katika mji huo kutokea kaskazini na kusini kwa ushirikiano wa vikosi vya aridhini, anga na majini.

Chapisha Maoni

0 Maoni