Wageni kutoka mataifa mbalimbali wanaotembelea eneo la
Hifadhi ya Ngorongoro wameendelea kufanya shughuli za utalii kwa amani, usalama
na utulivu na kufurahia vivutio mbalimbali vya utalii vilivyoko hifadhi ya
Ngorongoro.
Akizungumzia katika geti kuu la kuingia hifadhi ya
Ngorongoro Afisa Uhifadhi Mkuu Idara ya huduma za Utalii na Masoko Ngorongoro
Bw. Peter Makutian amesema kuwa katika kipindi chote cha uchaguzi mkuu wa
Tanzaia hadi kufikia jana tarehe 5 Novemba, 2025 wageni takribani 1200 kutoka
mataifa mbalimbali wameendelea kutembelea hifadhi hiyo na kufanya utalii.
“Ngorongoro tunaendelea kupokea wageni katika kipindi hiki cha msimu wa wastani na
tuna Imani kuelekea kipindi cha sikukuuu za mwisho wa mwaka watalii watakuwa
wengi zaidi .” alisema Makutian.
Mmoja wa wageni
kutoka Nchini Colombia Isabella Jerónimol ameeleza kuwa ametembeleaa Tanzania akiwa na
familia ya watu 26 ambapo chaguo lao ni
kuona hifadhi ya Ngorongoro kutokana na hali ya utulivu, amani, ukarimu pamoja
na utajiri wa vivutio vya utalii vilivyopo.
Bw. Dunstan Sospeter kutoka Dar es Salaam akiwa katika hifadhi ya Ngorongoro na Familia yake ameelezea kufurahishwa na hali ya usalama na kushuhudia utalii wa wanyamapori, uhifadhi endelevu, Wanyama mbalimbali ambao wanaweza kuonekana kwa pamoja katika muda ambapo pia ametumia fursa hiyo na familia yake kutembelea Bonde la Olduvai, mchanga unaohama na kreta ya Ngorongoro.


0 Maoni