Roboti yajichanganya na kumuua mfanyakazi ikidhania kuwa ni boksi

 

Mwanaume mmoja amekufa kwa kuminywa na roboti Korea Kusini, baada ya roboti kushindwa kumtofautisha mtu huyo na maboksi ya chakula iliyokuwa ikiyabeba.

Tukio hilo limetokea wakati mwanaume huyo mwenye miaka 40, muajiriwa wa kampuni inayotumia roboti alipokuwa akikagua utendaji kazi wa roboti.

Mkono wa roboti ulijichanganya na kudhani mtumishi huyo ni boksi la mbogamboga, na ilimnyanyua na kumkandamiza kwenye mkanda unaozunguka na kumpasua kichwa na kifua.

Mwanaume huyo alikimbizwa hospitali lakini taarifa za shirika la habari la Korea Kusini la Yonhap zimesema alifariki akiwa hospitali.

Kwa mujibu wa Yonhap, roboti hiyo ilikuwa inahusika katika kunyanyua maboksi ya karatasi na kuyapondaponda hadi kuyafanya kuwa punje punje.

Chapisha Maoni

0 Maoni