Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amemuapisha Dkt. Mwinyi Talib Haji kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.
Dkt. Mwinyi Talib Haji ameteuliwa tena kushika wadhifa huo baada ya kuutumikia katika kipindi kilichopita.
Tukio hilo limehudhuriwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Khamis Ramadhan Abdalla, Mhandisi Zena Ahmed Said (Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi), Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali na Dini.



0 Maoni