Mawaziri wa Fedha na
Mawaziri wa Jinsia barani Afrika wametakiwa kuhakikisha suala la kupambana na
ukatili wa kijinsia linawekwa kwenye Sera, mipango na bajeti za nchi ili
litekelezwe kikamilifu.
Waziri wa Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ametoa wito
huo jana Novemba 17, 2023 jijini Dar es Salaam wakati akifunga mkutano wa siku
tatu wa Mawaziri hao.
Amesema nchi zikiweka suala
la ukatili wa kijinsia kwenye Sera, mipango na bajeti itasaidia kufikia usawa
wa kijinsia kwa vitendo kama ilivyokusudiwa kwenye maazimio ya mikutano
mbalimbali na kuweza kuyapima utekelezaji wake.
Waziri Dkt. Gwajima amesema
masuala mengine ni kuwawezesha wanawake kiuchumi ili kuweka usawa na haki
katika umiliki wa rasilimali, ubunifu na teknolojia, ushiriki wa wanawake
katika masuala ya Amani na usalama ikiwemo kupata elimu kuhusu mabadiliko ya
tabia nchi pamoja na suala la Afya kwa wanawake.
Ameongeza kwamba Serikali ya
Tanzania imeshaanza kushirikiana na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
kuhakikisha masuala ya jinsia yanajumuishwa katika mipango na bajeti na
kukaguliwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi
wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF AfRITAC East) Dkt. Xiangming Li, amesema
washiriki wamehamasika na jinsi Tanzania inavyotekeleza suala la ushirikishwaji
wa wanawake kupitia uongozi thabiti wa Dkt. Samia Suluhu Hassan
Na. WMJJWM- Dar es Salaam
0 Maoni