Walioandamana kuiunga mkono Palestina waachiwa huru Kenya

 

Polisi nchini Kenya wamewaachia huru watu watatu waliowakamata kwa kushiriki maandamano ya kuiunga mkono Palestina, katika Jiji la Nairobi.

Waandamanaji hao wameachiwa huru Jumapili bila ya kufunguliwa mashtaka, baada ya Serikali kukosolewa mno na wanasiasa pamoja na makundi ya haki za binadamu.

Mbunge wa Kenya Yusuf Hassan alishutumu kitendo cha kukamatwa waandamanaji hao.

Mkuu wa Amnesty International nchini Kenya, Irungu Houghton amesema kuvuruga maandamano hayo ni kinyume cha sheria na ni kitendo cha kusikitisha mno.

Rais wa Kenya William Ruto alielezea msimamo wa Serikali yake wa kuiunga mkono kikamilifu Israel katika vita vinavyoendelea.

Chapisha Maoni

0 Maoni