Mashambulizi ya anga ya usiku ya Israel yauwa watu zaidi Gaza

 

Mashambulizi ya anga ya usiku mzima katika ukanda wa Gaza yamesababisha idadi kubwa ya vifo na majeruhi kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Palestina.

Wizara hiyo imeposti taarifa yake kupitia Telegram, ikisema kwamba mashambulizi hayo ya anga ni ya usiku wa jana na leo asubuhi.

Wizara pia imetoa picha ambazo zinaonyesha milipuko kwenye majengo na watoa huduma za dharura wakifukua miili ya watu kwenye vifusi baada mashambulzi.

Chapisha Maoni

0 Maoni