Kufuatia Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) kutabiri uwepo
wa mvua kubwa za mvua za vuli zitazokuwa na El Nino kuanzia katika mwezi huu wa
Oktoba hadi Desemba, Shirika la Bima (NIC) limewashauri wananchi kukatia bima
za nyumba zao ili kuzikinga na madhara yanayoweza kusababishwa na mvua hizo.
TMA walitoa tahadhari ya uwepo wa mvua ya El Nino
inayotokana na mabadiliko ya tabia nchi na kusema maeneo ya Pwani ya Kaskazini
na ukanda wa Ziwa Victoria yataathiriwa na mvua hizo, kwa kutambua umuhimu wa
wakazi wa maeneo hayo NIC imewashauri kukata bima ya nyumba zao ili pindi
yakitokea madhara waweze kulipwa na kuepuka kukosa makazi.
“Bima ya nyumba ni bima ambayo inalinda mmiliki wa nyumba
endapo nyumba yake inaweza kupata madhara yasiyodhurika mfano mafuriko au
imeungua moto wote tunasikiliza vyombo vya habari tumesikia kwamba kuna mvua
kubwa inategemewa kunyesha kwahiyo sisi kama NIC tunatoa wito kwa watu wakate
bima za nyumba kwa ajili ya kukinga nyumba zao endapo mvua kubwa itanyesha na
kuleta madhara kama mafuriko basi wasipate hasara na kuanza kuilalamikia
Serikali kuomba msaada wa nyumba zao kukumbwa na mafuriko wakate bima
itayosaidia kuwalipa na kujenga nyumba zao,” amesema Stella Marwa Meneja wa NIC
Kanda ya Ziwa.
0 Maoni