Winga Antony atemwa Brazil kwa tuhuma za ukatili wa kijinsi

 

Timu ya Taifa ya Brazil imemuacha winga wa Manchester United Antony, kufuatia kukabiliwa na tuhuma za ukatili wa kijinsia dhidi ya mpenzi wake wa zamani.

Shirikisho la Soka la Brazil limesema Antony mwenye miaka 23, ameondolewa kwenye kikosi cha taifa, baada ya kufahamika anachunguzwa kwa tuhuma hizo.

Chombo cha habari cha Brazil cha UOL, kilichapisha tuhuma hizo zilizotolewa na aliyekuwa mpenzi wa Antony, siku ya Jumatatu.

Polisi katika Jiji la Sao Paulo na wa Manchester wanachunguza madai hayo, ambayo hata hivyo mchezaji huyo ameyakanusha.

Chapisha Maoni

0 Maoni