Kim Jong Un kukutana na Rais Putin kuongelea msaada wa silaha

 

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un anapanga kwenda Urusi mwezi huu kukutana na Rais Vladimir Putin, afisa mmoja wa Marekani amesema.

Viongozi hao wawili wanatarajiwa kujadili kuhusu Korea Kaskazini kuipatia silaha Urusi kuiunga mkono katika vita yake na Ukraine.

Hata hivyo, haijajulikana dhahiri viongozi hao watakutana katika eneo gani. Pia, si Urusi ama Korea Kaskazini zilizothibitisha taarifa hizo, zilizoripotiwa pia na vyombo vya habari vya Marekani.

Chapisha Maoni

0 Maoni