Waziri Mkuu Majaliwa afanya kikao kazi na Naibu wake leo

 

Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa leo Septemba 6, 2023 amezungumza na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko katika kikao kazi kilichofanyika ofisini kwa Waziri Mkuu Mlimwa jijini Dodoma.

Kikao kazi hicho pia kilihudhuriwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama.

Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko walipokutana leo Septemba 6, 2023 katika kikao kazi kilichofanyika ofisini kwa Waziri Mkuu Mlimwa jijini Dodoma.

Chapisha Maoni

0 Maoni