Wauzaji wa mafuta rejareja Ukerewe watakiwa kuwa na leseni

 

Mkuu wa wilaya ya Ukerewe Hassan Bomboko amewataka wauzaji wa rejareja wa nishati ya mafuta kuzingatia sheria ya mwaka 2015 sura ya 393 kifungu namba 130 na 131 kinachotaka kuwa na leseni ya biashara hiyo.

Mkuu huyo wa wilaya ametoa kauli hiyo alipofanya ziara ya ukaguzi wa mafuta katika vituo vilivyopo kwenye wilaya hiyo ndipo akawataka wauzaji wa rejareja kuhakikisha wanakuwa na leseni ya biashara.

Katika hatua nyingine amewataka wauzaji wa nishati hiyo ya mafuta kutokuuza kiholela kwa walanguzi na wachuuzi wanaokwenda kutengeneza uhaba wa mafuta na kupandisha bei na badala yake wauze mafuta hayo kwa bei elekezi iliyotolewa na EWURA.

Chapisha Maoni

0 Maoni