Watu 50 wauawa katika shehere ya Maulid Pakistan

Watu wapatao 50 wameuawa na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa, katika shambulizi la kujitoa mhanga nchini Pakistan, polisi wamesema.

Mlipuko huo umetokea karibu na msikiti kusini magharibi mwa mkoa wa Balochistan Ijumaa, wakati watu walipokuwa wamekusanyika kusherehekea siku ya kusaliwa Mtume Muhammad.

Maafisa katika wa mkoa wa Balochistan wametangaza hali ya hatari. Hakuna kundi ambalo limedai kuhusika na shambulizi hilo.

Wakati huo huo, milipuko tofauti imetokea katika msikiti karibu na Mji Peshawar kwenye mkoa wa Khyber Pakhtunkhwa. Haijatolewa idadi ya walioathirika na tukio hilo.


Chapisha Maoni

0 Maoni