Tetemeko la ardhi laua watu 820 Morocco

 

Zaidi ya watu 820 wamekufa, baada ya kutokea tetemeko la ardhi lenye nguvu katika eneo la kati nchini Morocco, Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo imesema.

Tetemeko hilo lenye kipimo cha ukubwa wa alama 6.8, liliibua hali ya taharuki na kusababisha watu kukimbia katika mitaa ya Jiji la Marrakesh na katika miji mingine.

Vingi vya vifo hivyo vimetokea kwenye maeneo magumu kufikika ya mlimani, ambapo pia watu wengine wapatao 153 wamejeruhiwa.

Tetemeko hilo limetokea umbali wa kina cha kilomita 71, kusini magharibi mwa Marrakesh, kwa muijibu wa ripoti ya wanajiolojia.

Chapisha Maoni

0 Maoni