Chifu mwanasiasa Mangosuthu Buthelezi afariki dunia

 

Chifu muongeaji wa kabila la Wazulu, Mangosuthu Buthelezi, aliyetawala siasa za Afrika Kusini, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95.

Katika kipindi cha utawa wa kibaguzi wa makaburu Chifu Buthelezi, alianzisha chama cha Zulu Inkatha, baada ya kutengwa na chama cha African National Congress (ANC).

Maelfu ya wananchi wa Afrika Kusini waliuawa kwenye mapigano baina ya vyama hivyo viwili katika miaka ya mwanzoni mwa 1990.

Hata hivyo baadae Chifu Buthelezi alikaribishwa kwenye utawala wa Rais Nelson Mandela na kuhudumu nafasi ya Waziri wa Mambo ya Ndani.

Chapisha Maoni

0 Maoni