Rais Paul Kagame wa Rwanda, amethibitisha kuwania urais kwa
muhula wanne mwakani, jambo litakalomfanya kukaa madarakani kwa karibu miungo
mitatu.
"Nina furahishwa na imani waliyonayo kwangu raia wa
Rwanda,” Rais Kagame ameliambia jarida la lugha ya kifaransa la Jeune Afrique,
jumanne.
Mwezi Machi, Serikali ya Rwanda iliamua kuunganisha tarehe
za uchaguzi wa wabunge na wa rais kuwa siku moja, ambao unatarajiwa kufanyika
mwezi Agosti mwakani.
Kagame (65), aliingia madarakani mwaka 2000 kupitia kikundi
cha wapiganaji wa Rwandan Patriotic Front, kilichowaondoa Wahutu wenye misimamo
mikali waliosababisha mauaji ya kimbari.
0 Maoni