Wakazi wa mji wenye utulivu kusini mwa Hispania
wameshangazwa na kuibuka kwa picha za uchi za watoto wa kike, zinazotengenezwa
kwa kutumia teknolojia ya akili bandia (AI) na kusambazwa kwenye mitandao ya
kijamii.
Picha hizo za utupu zimekuwa zikitengenezwa zikiwalenga wasichana
ambao picha zao za awali walikuwa wamevaa nguo, na nyingi ya picha hizo
zilizobadilishwa kwa kutumia teknolojia hiyo ya AI zimetolewa kwenye akaunti
zao za mitandao ya kijamii.
Picha hizo huchakatwa kwa kutumia app ya kutengeneza umbo la
mtu mhusika bila ya kuwa na nguo, na kisha kusambazwa kwa nia ya kuwadhalilisha
na inasadikiwa kuwapo tukio la mmoja wapo kudaia atoa pesa ili picha yake isisambazwe.
Tayari watoto wa kike wapatao 20, wenye umri wa kuanzia
miaka 11 na 17 wamejitokeza kulalamikia kufanyiwa kitendo hicho cha matumizi
mabaya ya app hiyo, huko Almendralejo, kusini mashariki mwa mkoa wa Badajoz.
Polisi nchini Hispania wanachunguza taarifa hizo, ambapo wavulana
11 wamebainika kuhusika katika kutengeneza picha hizo za utupu ama kusambaza
picha hizo kwenye mitandao ya kijamii ya WhatsApp na Telegram.
CHANZO: BBC
0 Maoni