Mafuriko yaua maelfu ya watu nchini Libya

 

Maelfu ya watu wanahofiwa kufa baada ya mvua kubwa iliyoambatana na kimbunga kusababisha mafuriko nchini Libya.

Kiongozi wa serikali ya Libya ya mashariki, ambayo haitambuliki kimataifa, amesema watu waliokufa wanazidi 2000, na maelfu hawajulikani walipo.

Mtaalam wa Libya Jalel Harchaoui, ameliambia shirika la habari la BBC kwamba vifo vilivyotokea vinaweza kufikia maelfu ya watu.

Kimbunga Daniel kiliikumba Libya Jumapili, na kupelekea mamlaka za nchi hiyo kutangaza kuchukuliwa hali ya juu ya dharura.

Chapisha Maoni

0 Maoni