HALI TETE: Waliokufa kwa tetemeko la ardhi Morocco zaidi ya 2000

 

Waokoaji wanahaha kutafuta manusura kwenye vifusi baada ya tetemeko kubwa la ardhi lililoua watu zaidi ya 2000 nchini Morocco.

Katika eneo lililoathirika mno na tetemeko hilo la ardhi ni maene0 ya ndani ya mkoa wenye milima kusini-magharibi mwa Marrakesh, ambapo kijiji kizima nyumba zake zimeanguka.

Mwandishi wa kujitegemea wa BBC Nick Beake amefika katika moja ya kijiji, walichomkuta mwanamke mzee akipunga mkono kuomba msaada, baada ya miili ya watu 18 kupatikana.

Waokoaji wanahangaika kufikia maeneo ya ndani zaidi, huku nyingi ya barabara za mlimani zikiwa zimeharibika.

Kutokana na kuhofia kujirudia kwa tetemeko, wengi wa wananchi wa Morocco, wameamua kulala nje kwa usiku wa pili, wakilala mitaani.

Chapisha Maoni

0 Maoni