CCM Kwimba wampongeza Rais Samia kwa miradi ya maendeleo

 

Kamati ya siasa wilayani Kwimba mkoani Mwanza imeipongeza serikali kwa ujenzi wa miradi ya maendeleo katika wilaya hiyo na kusema itahakikisha inakaba kila eneo kuhakikisha wananchi wanapata huduma kama walivyowaahidi kwenye Ilani ya Chama  cha Mapinduzi CCM

Kamati hiyo ya wilaya ya Kwimba ikiongozwa na mwenyekiti wake Sabana Salinja imefika katika shule mpya ya msingi Mwalulyeho na kuridhishwa na ujenzi wake, na kuipongeza Serikali kwa kuwapunguzia wanafunzi adha ya kutembea umbali mrefu wa zaidi ya kilometa nane Kwenda katika shule ya msingi Chalasalawe

“Mimi Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi tupo hapa kwa ajili ya kuwatembelea na kukagua haya majengo mazuri mazuri yote yanayojengwa na CCM inachoongozwa na Rais Samia manmjua Rais Samia? Ndiyo huyu anayesababisha msome vizuri endeleeni kusoma mfike mbali baadae muwe mwenyekiti kama mimi,” amesema Sabana Salinja.

Akiwa ameongozana na Kamati hiyo ya siasa mkuu wa wilaya ya Kwimba Ng’wilabuzu Ludigija amesema ataendelea kusimamia miradi ya maendeleo kama ilani ya chama cha maoinduzi inavyoelekeza na kuwataka wanafunzi wa shule hiyo kusoma kwa bidii

“Zamani mlikuwa mnasomea Chasalawe mbali kutoka hapa lakini mmeletewa shule karibu ili msome vizuri sasa nawaomba muitunze vizuri na msome kwa bidi”.

Mohamed Felician na Mboje Kasomi ni wanafunzi wa shule hiyo wamempongeza Rais Samia kwa kuwajengea shule hiyo ambayo imewasaidia kuwapaunguzia kutembea umbali mrefu

“Tunamshukuru Rais Samia kwa kutujengea shule katika Kijiji chetu hapo mwanzo tulikuwa tunatembea umbali mrefu kwenda katika shule ya Chasalawe tulikuwa tunachoka sana lakini sasa tunasomea hapa hapa Kijijini kwetu ni karibu sana tunamuahidi Rais tutasoma kwa bidi na kufaulu” alisema mwanafunzi huyo.

Mimi online Tv

Chapisha Maoni

0 Maoni