Zaidi ya wakulima 600 wa kata ya Katunguru wilayani
Sengerema mkoani Mwanza wanatarajia kunufaika na mradi wa umwagiliaji
unaotarajiwa kukamilika mwezi Julai 2024 kwa gharama ya zaidi ya shilingi
milioni nne
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Sengerema Mwita
Waryuba akiwa na timu ya watalaamu wa halamashauri hiyo amewataka wasimamizi wa
mradi huo kuhakikisha wanashirikiana na jamii katika kutoa elimu ya
uhamasishaji wa mradi huo
“Mradi huu umeanza lakini hautakuwa na maana kama mtashindwa
kushirikiana na jamii inayowazunguka kwa kurudisha sehemu ya mnachokipata kwa
kuwezesha baadhi ya miradi kijijini hapa,” alisema Waryuba.
Kwa upande wake Meneja mradi huo Ombeni Ikola amewataka
wananchi hasa wafugaji wanaoishi kuzunguka eneo la mradi huo kutoingiza mifugo
kwenye eneo la mradi huo ili mradi ukamilike kwa wakati
Naye diwani wa kata ya Katunguru Sadick Jimola amemuomba
meneja mradi kuhakikisha taarifa za mradi zinawafikia wananchi ili kujua
kinachoendelea pamoja na kuzingatia kuungana na jamii kwenye masuala ya
uwajibikaji kwa jamii.
Mimi Online Tv
0 Maoni