Serikali ya Ufaransa imetenga kiasi cha dola za Marekani milioni
171.6 kuteketeza mvinyo wa ziada (wine) pamoja na kuwasaidia wazalishaji wa
mvinyo nchini humo.
Hatua hiyo inakuja kufuatia matatizo yanayoikabili sekta ya
mvinyo, yakiwamo ya kushuka kwa mahitaji ya mvinyo, kutokana na watu wengi kupendelea
kunywa bia.
Uzalishaji mvinyo kwa wingi pamoja na kupanda kwa gharama za
maisha pia vinaikabili sekta ya uzalishaji mvinyo nchini Ufaransa.
Idadi kubwa ya fedha iliyotengwa, itatumika kununua mvinyo wa
ziada na pombe iliyomo kuuzwa kama bidhaa za vitakasa mikono (sanitizer),
bidhaa za kusafishia pamoja na manukato (perfume).
0 Maoni