INEC yamuengua tena Mpina kwenye mbio za kuwania urais

 

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imekubali pingamizi lililowasilishwa Mwanasheri Mkuu wa Serikali dhidi ya uteuzi wa Mgombea urais wa ACT-Wazalendo Luhaga Joelson Mpina na kutupilia mbali mapingamizi mengine matatu.

Taarifa ya Mkurugenzi wa Uchaguzi INEC Kailima Ramadhani Kailima, imesema, hivyo INEC imemuondoa Mpina wa ACT-Wazalendo kwenye orodha ya wagombea wa kiti cah Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Pingamizi hilo la Mwanasheria Mkuu wa Serikali, limekubaliwa na INEC huku ikitupiliambali mapingamizi mengine mawili dhidi ya Mpina na moja dhidi ya Mgombea Urais wa CCM Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alilowekewa Mpina wa  ACT-Wazalendo.

Hatua hiyo inakuja ikiwa ni siku chache tu kupita tangu, Mahakama Kuu kuamuru Mpina arejeshe fomu za uchauzi INEC ambapo alifanyahivyo na kurejeshwa kwenye mbio za uchaguzi lakini hata kabla hajaanza kampeni ameenguliwa tena.





Chapisha Maoni

0 Maoni