Mwanariadha Alphonce Felix Simbu wa Tanzania ametwaa medali ya dhahabu
kwenye mbio za marathon kwa ushindi wa kusisimua dhidi ya Amanal Petros wa
Ujerumani jijini Tokyo, siku ya Jumatatu.
Simbu na Petros, ambaye alizaliwa Eritrea, walikimbia kwa
muda sawa wa saa 2, dakika 9 na sekunde 48, lakini Simbu alionekana kupiga
hatua ya mwisho kwa kasi zaidi, akimaliza mbele kwa tofauti ya sehemu tatu za
sekunde (0.03), katika hitimisho la kusisimua la tukio refu zaidi kwenye
Mashindano ya Dunia yaliyofanyika katika mji mkuu wa Japan.
Iliass Aouani wa Italia alishika nafasi ya tatu na kutwaa
medali ya shaba kwa muda wa 2:09:53.
"Leo nimeandika historia – dhahabu ya kwanza kwa Tanzania kwenye mashindano ya dunia," alisema Simbu, ambaye aliwahi kushinda medali ya shaba katika Mashindano ya Dunia ya mwaka 2017 jijini London.


0 Maoni